Joshua 21:20-22

20Koo nyingine za Wakohathi, ambao pia ni Walawi, walipewa miji kutoka kabila la Efraimu: 21 aKatika nchi ya vilima ya Efraimu walipewa Shekemu (mji mkubwa wa makimbilio kwa yeyote anayeshtakiwa kwa mauaji) na Gezeri, 22 bKibsaimu na Beth-Horoni, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji minne.
Copyright information for SwhKC